Jukumu Maalum Kutoka Kwa Mungu

Jukumu maalum kutoka kwa Mungu

Na Daniel Parkes

Kitabu cha Ufunuo kinanena juu ya mashaidi wawili watakaubiri wakati wa dhiki kuu. Unaweza kusoma juu ya haya katika Ufunuo 11:3 – 12. Nitanukuu hizo aya hapa;

“Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magurua. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili. visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutatoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.”

(Ufunuo 11:3 – 6)

“Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule myama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho sodoma na misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa. Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. Wao wakaao juu ya nchi wafuruhi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.”

(Ufunuo 11:7 – 10)

“Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai iitakayo kwa mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao, na hofu kuu ikawangukia watu waliowatazama. Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, pandani hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu adui zao wakiwatazama.”

(Ufunuo 11:11 – 12)

Tunajua kutoka Ufunuo 11:3 kuwa hawa mashadi wawili watatoa unabii kuwa siku 1260 (hiyo ni miaka 3.5 ukitumia kalenda ya Kiyaudi yenye siku 360 kwa mwaka). Hii ni hakika pia hukitegemea Ufunuo 11:2 ambayo inahesabu miaka 3.5 kama “miezi arobaini na mbili.” (Tena zaidi miaka 3.5 ya Ufunuo 11.2 inaonekana ikikubaliana na miaka 3.5 ya Ufunuo 11:3 na ninafikiri ikikubariana hivyo ni sawa.)

Kwa njia nyingine, ukitegemea Ufunuo 11:2 -3 ile njia ya kuelewa hesabu ya kiunabii kuwa siku moja inazimamia mwaka. Vile vile inavyotumika katika kitabu cha Danieli hapa hatumiki. Tunjukua nyakati zilizonenwa katika Ufunuo 11:2 – 3 kama za kawida tu.

Katika haya ya 7 hao mashahidi wanauawa. Lakini, “baada ya siku tatu unusu, roho ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingi na wakasimama na miguu ya na wakapaa juu mbinguni katika wingu.” Hivyo basi mashahidi walifufuliwa na wakanyakuliwa. Angalia kwa “makini nini kinafanyika. Wanafufuliwa katika 1 Watesaloniki 4:16b yaani wananyakuliwa kama vile “sisi tulio hai na tumebaki.” Tutakavyonyakuliwa katika Wathesalonike I 4: 179. Haya kweli ni mambo tofauti ambayo hayapatikani mahali popote katika maandiko. Kwa mfano katika kisa cha Enoku, yeye “ananyakuliwa” lakini hakufufuliwa (kwa sababu hakufa). Hii pia ni kweli katika kisa cha Elijah. Na hii pia ni kweli kwa waumini wote watakaonyakuliwa siku ya mwisho wakiwa hai.Lakini, kwa sababu tu nyingine, hawa mashahidi wawili wamechukuliwa kwa njia maalaum hata zaidi ya yale yatakao wapata wakristo wengine ambao watauawa wakati wa dhiki kuu (Ufunuo 20:4). Swali langu ni kwanini? Wale wakubali kuwa wakristo katika wakati wa dhiki kuu hawataipata mili yao mpaka baada ya wakati wa dhiki kuu. Hii ni wazi kutoka ufunuo 20:4b ambayo inasema, “Kisha nikaona viti vya enzi wakakehi juu yake nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho za waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la mungu na hao wasiomsujudia yule myama wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai wakatawala pamoja na kristo miaka elfu.” (Ufunuo 20:4). Haya hii inafundisha vile mamba yatakavyokuwa baada ya dhiki kuu. Lakini hawa mashahidi wawili wanapewa kibali maalum. Kwanza wanafufulia kabla ya wakati wa dhiki kuisha. Tunajuaje? Hii ni kwa sababu tunasoma baada ya kunyakuliwa kwao hivi. Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi na sehemu ya kumi ya maji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu wakamtukuza mungu wa mbingu” (Ufunuo 11:13). Hapa hakuna ushahidi kwamba wakati wa dhiki umeisha wala hakuna kutachwa kwa wale waliouwa wakati wa dhiki kuu kufufuliwa. Ni wale mashahidi tu!

Baada ya wale mashahidi wawili kunyakuliwa tunasoma, “Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi.” (Ufunuo 11:14). Hukumu zaidi zinafuata. Nyakati za dhiki hazijakwisha bado. Lakini hawa mashahidi wawili walikuwa ni waumini kabla ya nyakati za dhiki kuu na kweli ingebidi wangoje pia sawasawa na wengine mpaka siku ya unyakuzi, lakini jua kwamba hawa walipewa “Kazi maalum na bwana.”

Sasa wakati mtu anapewa jukumu maalum huko anakofanya kazi anapewa hili jukumu kwa muda gani? Jibu ni wazi na rahisi. Mpka amalize lile jukumu maalum. Sasa hawa mashahidi wawili walipewa kazi maalum kwa muda gani? Kazi yao ilikuwa ya siku tatu unusu baada ya hapo waje. Pengine hii ilifanyika hili ilingane na vile Bwana wao alikaa kaburini baada ya kuuawa kinyama na bwana anataka tutumie hii kusaidia dunia yote kuelewa. Pengine “nusu siku” imeongezwa kwa siku tatu ili kila mtu ajue wamekufa siku tatu ili ilingine na vile bwana yesu alisema mwili wao utakaa kaburini “Siku tatu na usiku” ninaweza kukusikia tu vile vichwa vya habari ya dunia vitakavyo lipuka na habari wakati huo. “wanaume wawili wafufuke wafu baada ya siku tatu.” Haitachukua dakika nyngi kabla hiyo habari kuzambaa duniani kote! Sio ajabu aya iliyofuata inasema, “Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nci, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka wanadamu elfu saba wakauwa katika tetemeko lili. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu” Ufunuo 11:13.

Ah, sasa tunaelekea mahali; sasa mtu hatimaye amekubali kusikiza. Hao mashahidi wawili watatumiwa na Mungu kwa njia ya nguvu sana. Kwa hakika wale mashahidi wawili wanastahili kunyakuliwa, kwa sababu walihitimu mbele yawengine wote. Walikuwa ni wakristo kabla ya dhiki kuu (na hivyo basi kabla ya unyakuzi). Lakini walipewa jukumu maalum kutoka kwa Bwana.

Fundisho hili limetafuziliwa na Jeremiah M. Mosomi.

Tarehe: 26/07/2011

Leave a Comment